Karibu kwenye shindano la Dijito 25’ linalowaunganisha wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Tanzania ili kushindana, kujifunza na kuunda suluhisho bunifu za kijamii na kibiashara. Hii ni nafasi yako ya kukuza biashara yako na kuleta mabadiliko chanya katika jamii yako.
Dijito 25’ ni shindano linalolenga kukuza vijana katika ujasiriamali kwa kidigitali, ubunifu wa bidhaa, na teknolojia. Washiriki wataelezea biashara zao zinatatua changamoto zipi katika jamii zao.
-> Huduma bure ya graphics design & branding
-> Fursa ya mentorship kukuza biashara
Tunawawezesha vijana kwa maarifa na zana za ubunifu ili kubadili kukuza biashara na miradi yao. Kila shindano linawaunganisha wabunifu, mawinga, wajasiriamali na wanafunzi mbalimbali.
Maombi ya Dijito 25' Challenge yataanza tarehe 7 Oktoba 2025 hadi tarehe 12 Oktoba 2025. Unaweza kujisajili kupitia: Hapa
Baada ya dirisha la maombi kufungwa, maombi yote yatahakikiwa. Mchakato utajumuisha kuhakiki taarifa za biashara na kutathmini ubunifu wa biashara husika.
Waombaji watakaofanikiwa kupita hatua ya uhakiki watachakatwa kupata wajasiriamali bora.
Wajasiriamali watakaoshinda watapata huduma ya bure ya graphics design kutoka Dijito Frames na fursa za ushirikiano siku za mbeleni.
Tumeanzishwa chini ya Dijito Frames kwa lengo la kujenga kizazi kipya cha wabunifu na wajasiriamali wanaotumia teknolojia kama chombo cha maendeleo. Kila mwezi tunazindua changamoto mpya inayolenga sekta tofauti kutoka ubunifu wa kidigitali hadi teknolojia ya kijamii.